Wednesday, May 5, 2010

Magazeti ya Zanzibar


Wafanyakazi wa Government Press 1950

Office Gazet, Marifa, Madhukari, Mkombozi, Mwiba, Mwangaza, Mkulima, Nyuki, Ruta + Ruta, Afrika Kwetu, Adal Insaf, Agope, Agoze, Alfalak, Alnahadha, Altarika, Habari za Wiki, Jamhuri, Jasho letu, Kibaruwa, King George, The VISCH . M, Kipanga, Samachar, Daily Commercial Report, British Imformation Serv, Normal Magazine, Mazungumzo ya walimu n.k.

Monday, February 15, 2010

Uchimbaji wa mafuta Zanzibar

 
Syd.Khalifa akiikagua mitambo ya kuchimba Mafuta, Zanzibar pamoja naye ni M.M.Pennel wa Mkuu wa Kampuni ya Shell.
 
Kutafuta mafuta Zanzibar kumeanza mwaka 1957, ilitarajiwa kisima cha Chuwini peke yake kitachimbwa kufikia futi 12,000, ukiwachilia sehemu nyingine kama Charawe
 

Mtambo wa
kutafuta Mafuta Kisiwa cha Unguja

Seyyid Khalifa bin Harub


Jina lake hasa ni Syd Khalifa bin Harub bin Thuwein bin Said bin Sultan bin Imam Ahmed bin Said bin Mohammed bin Ahmed bin Khelef bin Said Al Azdy.
Kama kisambare Syd Khalifa alizaliwa akiwa kapiga rangi ya ubulu, kitu kilowatisha wakunga na watu wazima waliokuweko,  na wakanza kunong’ona, labda alijizonga na kitovu, labda kapata kisonge, labda subian labda labda labda, lakini kila siku kupita alirudisha ile rangi yake ya Kiafrika kama ya wazee wake. 

Sunday, January 17, 2010

Buibui la kizanzibari


Wanawake wa Kizanzibari na mabuibui


Buibui linasafari refu kutoka huko lilikotoka huko kwao Iran, lilikuwa na lengo moja tu nalo ni kustiri, na ahadi hiyo ninanvyoona mimi inaitekeleza, ikiwa mwanamke analolivaa anahishima au laa, halijali kazi yake kubwa ni kumstiri mvaaji na kumpa heshma. Kabla ya buibui hili la kamba, hapa Zanzibar pakivaliwa buibui la lembwani, ni guo refu la silk, wakivaa wanawake wenye uwezo tu, tena wakijifunika gubi gubi, hasa wanawake wa kishirazi walokuwa na uwezo, likivaliwa sana pande za Hurumzi, ama lilipotea baada ya kuingia barkowa, wanawake wengi wakiiga Waarabu Kutoka Oman, Kuweit, Baharein n.k.

Saturday, January 16, 2010

Bi khole


Bi Khole katika mapozi yake

 Bibi mzuri bi Khole bint Said Sultan bin Imam Ahmed [Al Azdy] inasemekana alizaliwa 1828, mtoto wa pande la mama la kiashuria [Assyrian] – Najmu Sabah aliemzaa mtoto ndie, kwani yeye ndie aliyekuwa kama Miss Zanzibar zama zake, na si kwa uzuri tu ni kwa sifa nyingi za kiwanajike, alikuwa si mwanamke rahisi kuchezelewa, alikuwa anaijuwa hadhi na kima chake,