Bi Khole katika mapozi yake
Bibi mzuri bi Khole bint Said Sultan bin Imam Ahmed [Al Azdy] inasemekana alizaliwa 1828, mtoto wa pande la mama la kiashuria [Assyrian] – Najmu Sabah aliemzaa mtoto ndie, kwani yeye ndie aliyekuwa kama Miss Zanzibar zama zake, na si kwa uzuri tu ni kwa sifa nyingi za kiwanajike, alikuwa si mwanamke rahisi kuchezelewa, alikuwa anaijuwa hadhi na kima chake,
alikuwa kakaza kazi nyingi za babake akizishulikia mwenyewe, hiyo ndio sababu kubwa mkasikia kuwa Said Sultan alifanikiwa kiutawala ukiwa na watoto kama hao unategemea nini, si watoto watakaombuhudhi mzee mpaka wakamtowa roho ndio wajitie kulia na kuomboleza. Najum Sabah alimzalia Sultan watoto watatu, yaani Bi Aysha, Seyyid Hilal na Bi Khole. Na yeye ndie aliyekuwa na amri zote za nyumba kubwa Baytil-Sahil, kwa vile alikuwa mpambe Bwana Said alikuwa kapowa, alipokufa mama yake ndipo alipowachiwa yeye Khole upambe wa nyumba na akamshinda mama yake akifahamisha kipi kiwekwe wapi na kile kiwekwe vipi, na mionzi ya historia lazima imguse kwani alimshauri baba yake mambo mengi yalosaidia kuipa jina Zanzibar, kwa hivyo usifikiri kuwa alipendwa bure, kitu kilomfanya dada yake Aysha amuonee wivu na kumpigia makelele ya amri kila mara, si hayo tu hata uvaaji wake ni mzuri wa hishma na uchaguzi mzuri wa vitambaa maridadi vya cotton n.k vinavyolingana na hali ya hewa ya hapa Zanzibar mara nyingi akifananishwa na malkia .
Kuna hadithi inayosema kuwa kuna Muarabu alikuwa akicheza Zarha [kucheza na mapanga] kwenye kiwanja cha Beit el Sahil, walipokuwa wakileta kinara kwa Sultan kwa fadhaa alijichoma kwa panga kidevuni bila ya khabari alitahamaki damu zikimtiririka, kisa kamuona Bi Khole na kuna pokezi nyengine kuwa aliumia mguu kwa mkuki sikuweza kuiwacha hadithi hii kwani ilikuwa marufu sana wakati wa zamani. Aliwahi kumlea Seyyed Abdull Aziz mtoto wa 13 wa kiume wa Seyyid Said baada ya kufariki mama yake, lakini kwa bahati mbaya, kwa vile alikuwa na bi Aysha ambae alikuwa mkali kwa Khole mtoto huyo alinyanyukia kupenda sana vita na choko choko, na walimuunga mkono mara moja Seyyid Barghash katika vita kwa vile Khole alikuwa pamoja nae na wakampiga pande kaka yao Seyyid Majid. Kwa hivyo haifai kufanya mambo ovyo ovyo mbele ya watoto.Alirithi kwa baba yake Shamba kubwa la kizimbani, aloliendeleza wala halijamkunyuwa kidole na akawanyamazisha viyengele yote waliosema litamshinda mtoto wa mjini . Kingo yake ilizimika na kukata roho mwaka mwaka 1875 sawa sawa na 1292 A.H, katika nyumba alikokuwa akiishi baadae Beity Thani, nyumba ya marehemu baba yake aliyemjengea mkewe wa Kiajemi [habari zake zitakuja siku nyingine] kifo kilomuacha kaka Barghash hoi kwa msiba na asiwe na wakumlalamikia na kumpa kila cha tunu na tamasha, Saide Salme asiwe na wakumueleza ya undani hata dunia ikampiga akaritadi, huyu si Khole wa miembe mingi, wala Khole aliyeolewa akaacha mtoto, alikuwa muaminifu alikataa mapema jukumu la ndoa asioliweza, sikama wengi wanavyofikiria kuwa ndowa ni jambo jepesi, kesho utaulizwa mke, mume na watoto umezifanya nini haki zao, kama itakavyoulizwa zinaa. Nadhani hata ukimfukuwa leo Khole mafupa yake ni bakira, kwa maelezo yake mengi ya undani niliyoyapata hajaguswa si jina chafu analopakazwa.

This comment has been removed by the author.
ReplyDeleteShukran
ReplyDeleteNa kuna uwiyano upi baina ya bi khole huyu na maelezo ya bi khole anaelezewa bungi?
Ndo huyohuyo mwanzo alikuwa anaishi Bububu baadae akahama akahamia Bungi. Historia inaeleza hivyo
DeleteAlhmamdulah
ReplyDeleteLeo nimepata ukweli wa dhana yangu ya ukweli Alhmamdulah nimelifurahia mimi na khamas_g
Alhmamdulah
ReplyDeleteLeo nimepata ukweli wa dhana yangu ya ukweli Alhmamdulah nimelifurahia mimi na khamas_g
MBONA HABARI KAMA ZAKINZANA AMA SIKUFHAMU ? HII PICHA HAPA NI YA BI KHOLE AMA PRINCESS SALME ?
ReplyDeleteKwa kweli zanzibar ina historia kubwa na imeondokewa na watawala wazuri na si rahisi kurudi tena katika neema zake lakini kwake Allah swt yanamuelewa na tunamuomba airudishie neema zake amin
ReplyDelete