Jina lake hasa ni Syd Khalifa bin Harub bin Thuwein bin Said bin Sultan bin Imam Ahmed bin Said bin Mohammed bin Ahmed bin Khelef bin Said Al Azdy.
Kama kisambare Syd Khalifa alizaliwa akiwa kapiga rangi ya ubulu, kitu kilowatisha wakunga na watu wazima waliokuweko, na wakanza kunong’ona, labda alijizonga na kitovu, labda kapata kisonge, labda subian labda labda labda, lakini kila siku kupita alirudisha ile rangi yake ya Kiafrika kama ya wazee wake.
Ingawa alizaliwa Oman siku ya tarehe 26 mwezi wa Agosti mwaka 1879, mama yake toka hapo afya yake ikawa mbaya na yeye akafa na akawachwa Khalifa ni yatima, wa baba na mama. Ikabidi aondolewe kwao apelekwe kulelewa kwenye kasri ya Sultan Syd Feisal bin Turki, ambae ndie mjomba wake nae ndie Sultan wa Muskat.
Na Bwana huyu kufikia umri wa miaka 13 alilazimika kuja Unguja aje aitikie wito wa ami yake Syd Hemed bin Thuwein, aliyekuwa mfalme wa Zanzibar wakati huo, aliyetawala mwaka 1893 mpaka mwaka 1896
Kwa hivyo yeye ni mjukuu khalisi wa Syd Thuwein, aliyetawala Oman, ambae Mwenyezi Mungu Alimtunukia watoto wengi , akiwemo Syd Harub na Syd
Hemed. Na Syd Harub alikufa akiwa kijana sana.
Baada ya kufa baba yake Syd Khalifa alilelewa na babu yake Syd Turky na alilelewa pamoja na mjukuu mwengine wa Syd Turky yaani Syd Taimur na walilelewa kishujaa na mafunzo kede kede mpaka akapikika na alipokuja huku Zanzibar akazidi kuwa mahiri na mtaalam wa mengi, hasa farasi. Siku aliyokuja hakuna
mtu yoyote aliyejuwa aliingia ghafla katika mwaka 1903, na meli aliokuja nayo ikiitwa Aboukir kabla ya kuja Zanzibar alipitia Makka kwa ajili ya ibada ya Umra, mara ya pili alikwenda na shemeji yake Syd Ali , na huko ndiko alipokutana na mkewe bi Matuka na wakapendana, ambae naye yeye alifuatana na harimu yake, kaka Ali bin Humud ambae nae pia aliwahi kuwa Sultan wa Zanzibar Syd Khalifa aligota milango mingi ikiwemo hata ya mambo ya michezo kama ya sailing, polo, tennis na milango kadha wakadha ya kidunia na ya kiakhera [Dini] alimradi aliishi. Alihudhuria mabaraza mengi sana akiwa
bado mtoto, kitu kilompelekea kuwa kiongozi mzuri baadae, na kumudu kukaa kwenye kiti cha usultani kwa muda mrefu zaidi.
Syd Khalifa alipata watoto wawili, baada ya kufa mmoja alizaliwa Syd Prince Sir Abdalla 12 feb 1910. na alipokufa Bi Matuka Ndipo alipomuowa Bi Nunuu binti Ahmed. Alitawala tarehe 9 Disember mwaka 1911 , na yeye ni miaka 32, ingawa kiti hicho ilikuwa atawale Syd Khalid bin Muhammed,
lakini Bwana huyu alikataa kata kata kutawala na akajitia maradhi.
Na moja ya kazi yake kubwa alitufunguwa uso Wazanzibari kwa kuwasaidia Waingereza katika vita viwili vikuu.
No comments:
Post a Comment