Saturday, January 16, 2010

Dar es Salaam,Zanzibar




JEE UNAJUWA KAMA DAR-ES-SAALAM
IMEJENGWA NA WAZANZIBARI ?, 
 Dar-es-salaam inatokana na neno la kiarabu bandar salaam jina hilo linatoka na mji mmoja ulioko Iraq, ulianza kuwa mji baada ya kufyekwa msitu kwenye ghuba ya Chokir na watu waliotoka Zanzibzr wenye asili ya Barawa [Somali] na Shirazi ili wapate nafasi nzuri ya kutumia bandari walikuwa wakitengeneza mitumbwi, wakivuwa na baadae wakahamia,
kikaanza kuwa ni kituo chao cha safari za biashara makaazi hayo waliyaita mzizima yaliyoanzia ghuba ya chokir kwenye ufukwe wa bahari kati ya Msasani na Magogoni karibu ya ikulu [Ferry] ingawa kulikuwapo makaazi kwenye fukwe za bahari kuanzia Kunduchi hadi Mbwamaji Kigamboni ambayo iko kusini mashariki ya Dar-es-salaam halafu watu hao walikuja kujulikana kama washomvi asili ya kuitwa hivyo aliwahi kuja Muyemen mmoja na jahazi ya shehena kubwa ya chumvi aliyeitwa Mohamed bin Saleh el-Hatmy na washirazi walimkaribisha na wakamuozesha mke bi Makazija mtoto wa kiongozi wa kishirazi aliyechanganya na uwenyeji, na hapo palipatikana kizazi cha shomvi, na bwana Mohammed el-hatmy alikuwa akiwatuma watoto wake wakisafiri wakileta chumvi mnamo mwaka 1860, walitumia chumvi hiyo kuwarubuni Wazaramo wawapige wakamba waliokuja kutoka Kenya kuhujumu Dar-es-salaam, wakati huo chumvi ilikuwa na thamani sana.  Na upande wa Wazaramo walikuwa na kiongozi wao akiitwa Pazi Kilama [kibamandu, kihamanduka] aliekuwa shujaa sana na aliejulikana toka Ukuru mpaka Zaramo waliposikia kuna wakamba wamefanya vita na kuwanyan’ganya jirani zao washomvi, wakakimbia na kuhamia visiwani walikasirika na kuna baadhi ya Wabarawa walikimbilia Zaramo, mtu aliekuwa akiwasaidia sana akiitwa Makalisani alianza nao biashara ya shanga, nguo na chumvi. Makalisani yeye na wabarawa ndio waliomshauri Pazi kwenda kuwapiga wakamba, Pazi akamtuma Mtandile aliekuwa na mke wa pili Dar-es-salaam aende kuchunguza na akaleta habari mbaya za ufisadi uliofanywa huko na Wabarawa wakatoa ahadi ya kumpa makanda ya chumvi zaidi, Pazi akaitsha mkutano wa vita akafanya tambiko lililoitwa vumba, wakaenda vitani na kwa bahati nzuri wakashinda na kukawa na amani kuliko Bagamoyo ambako kulikuwa na upinzani wa Wazaramo chini ya uongozi wa Pazi. 1865 mji ulianza kujengwa rasmi na Sayyed Majid na yeye mwenyewe alikwenda kwa mara ya kwanza 1886 na kaimu wa Uingereza wa Zanzibar Sir Seward, na alimuweka Seyyid Mansab kuwa kadhi mkuu wa Dar, Majid alikufa kabla ya kumaliza kujengwa kwa mji huu, na Barghsh alipotawala hakutilia maanani kwani alikuwa hasimu yake mkubwa, na wafanya biashara wengi wakarejea Unguja na serikali ya Kiingereza ambayo ilikuwa na koloni yake Malawi ikaanzisha ujenzi wa barabara kati ya pwani na ziwa nyasa ulosimamiwa na Sir William Mackinnon, ingawa wakisaidiwa na mpelelezi Karl Peter alifika pande hizi mnamo mwaka 1885 akawarubuni machifu na wakamkukubalia atumie bandari ya Dar, zama hizo Dar kulikuwa na wakaazi karibu ya elfu nne. Februari 23 1886 walikuja wajumbe wakiongozwa na Kanali Kit Chener kuja kupunguza mipaka ya sultani wa Zanzibar iliopo bara na wakati huo kulikuwa na liwali Muhammed bin Suleiman El-Haroun kutoka Oman. Mwaka hou huo manuari za kivita zilikuja Zanzibar kupata mkataba wa kibiashara kutoka kwa sultani wakitumia ule mkataba walioupata kutoka kwa machifu na Karl Peter. Mnamo mwaka 1887 Muingereza na Mjerumani walitiana saini kuhusu mwambao, mwaka huo huo Lene ambae ni muwakilishi wa kampuni ya Kijerumani E.A, walikuja na wasaidizi na wapagazi aliopewa na sultani Barghash waliotoka Zanzibar kuja kuwasaidia, na wenyeji waliwapokea vizuri na kufiki katika nyumba zilizojengwa na Seyyid Majid baadae aliwasihi wahindi wengi wahamie huko na wakaanza biashara na kujenga majumba, na kama utatizama majumba mengi ya mjini Dar yameandikwa ya wazanzibari. ‘Tunawaambia watani wetu wa Kimrima kuwa hawataipata Zanzibar ng’o! na hata bara ni yetu Wazanzibari. Musitake mambo’ [utani wetu wa kijadi].

1 comment:

  1. Nafikiri bado hujachimba vyema kuhusu history Za Tanzania haswa hii ukweli unachanganya na siasa acha u CUF pembeni andika vitu vya ukweli.

    ReplyDelete