Thursday, January 14, 2010

Mambo msiige



ASILI YA UJENZI WA JUMBA LA MAMBO MSIIGE

Ujenzi wa mambo msige ni mashindano ya kifahari ya Bwana Salum Bin Issa Al-Baruwan  na matajiri wenzake wawili na yeye aliingia kwa kuunda meli mbili kubwa za matanga akaziita Harthiya na Salhiya na mwenziwe Bwana Suleiman Habib yeye aliingia kwa kujenga jumba kubwa pale Malindi Funguni pale mwanzo wa Hollies road (Barabara ya kwendea Bububu) kwa siku za nyuma pakijulikana kama mkahawani
au jaa la Suleiman Habib, maana ya kuwa jaa ile nyumba yake ilititia kwenye kinamasi (matope)  mwenzao aliyeshindana nao ni Bw. Salum bin Harith na yeye ndiye aliyejenga nyumba hii ya Mambomsige alijenga mwaka 1850 na inasemekana baadhi ya udongo wake ulipondwa kwa ute wa mayai na ndio pakasemwa “Mambo Msiige”  na isonekane ajabu wakati huo Zanzibar ilikuwa na neema nyingi.


Wataalamu mahiri wa ujenzi na waliiga mfano wa ujenzi wa jumba la kifalme la uchina, lilijengwa jumba hilo pale hasa penye umbwe (ufukwe) wa rasi Shangani, hapo ndipo hasa watu wa Mji wakija na mafarasi yao wakifanya harusi zao,pia mwaka kwa mwaka na kila mwaka pakifanyiwa resi za ngarawa na pakikogwa mwaka, Siku ya ufunguzi wa jumba hili hata mwenyewe Sayyid Said alihudhuria.Iliwahi kukodishwa Mambo Msiige kwa Bishop toper na Bishop Steere katika mwaka 1864 na iliwahi kujulikana jumba hili kama jumba la ukufuru wenyeji labda wakimaanisha kule kuritadishwa kwa waislamu watano ndani yake, yaani jumba la Mission, mpaka walipojenga Mkunazini 1874 na aliwahi kukaa Sir John Kirk Consol General mwaka 1875 na mwaka 1873 na 1887 H.M. Stainley alikaa humo mara mbili na chumba cha juu kabisa kilitengenezwa vizuri kwa ajili yake. Inasikitisha kuona kule juu sasa wamehamia ndege vipasua sanda (Bird of evil Omen). Hapo pangekuwa kivutio kikubwa kwa watalii.Mwaka 1913  - 1924 jumba hili lilikuwa Hospital ya Wazungu, lilikuwa na mlango mkubwa mzuri ambao ulitolewa ukapelekwa jumba la ndege.

No comments:

Post a Comment