Thursday, January 14, 2010

Princess Salme.



BINTI MFALME ALIYEIUZA ZANZIBAR NA DINI YAKE KWA MAPENZI

Salme mtoto wakike aliye kuwa sheshe na taji wa Sayyed Said Bin Sultan alizaliwa saa 3 usiku august 30th 1844 na mama aliyekuwa suriya mzungu mtumwa wa kisharkasia (circassians) aliyekuwa jamaa wa mama yake Sayeed Majid.

Alipokufa mama yake yeye ndiye aliye mlea, walihamia mjini na mama yake alivyokua na umri wa miaka saba walikaa bait-el-Sahil mpaka alipo kufa baba yake akatawala Sayeed Majid akiishi na dada yake Bikhole, yeye na khole waliwahi kuwa mahasimu na Sayeed Majid wakampendelea sana Baraghash, mpaka wakamtorosha alipofungwa. Kwa baba yake alirithi shamba la kizimbani na aliwahi kuka huko, mwisho walihamia nyuma ya Ng’omekongwe, mama yake alikufa mwaka 1859 kwa maradhi ya kipindupindu,alisalia peke yake katika nyumba hiyo alipotimia miaka 16 alipata mimba nje ya ndoa ya jirani yake  Henrrch Riute karani wa kijerumani aliyekuwa akiifanyia kazi kampuni ya HAUSING & CO. jambo hilo lilimtia wasi wasi nalingelijulikana ingekuwa aibu na fedheha kubwa kwa nchi nzima alimwandikia barua ya kuhuzunisha akampelekea kepteni wa manuari ya kiingereza iliyokua ikiitwa H.M.S highfligher iliyokuwa iko bandarini alimuomba amchukue ili ikijulikana itakuwa mtihani na mtafaruku mkubwa baada ya kepteni kuzingatia kwa makini tukio zima na hatari inayo mkabili bibie, akaamua amsaidie, ikangojwa siku ya kukoga mwaka Octoba 26 1866 siku ambayo wanawake wengi wa Unguja walikuwa wakicheza ngoma itwayo Shindwe ilikuwa ikichezwa kwa kuwafungia milango wanaume kwa nje mtindo ujulikanao kuwasha moto,ilitayarishwa kihori na watumwa wake wawili Jahuri na Bakari walipofika kwenye manuari alishushiwa ngazi akapanda upesi upesi pale pale waliondoka akiwawacha wale watumwa hoi wakipiga makelele wakidhani aliibiwa alipofika Aden (Yemen) alishuka akimngoja mchumba wake wakijerumani wakakutana na akamletea vitu vyake vyote muhimu alivyoviwacha nyuma alibadilisha dini akajiita Emily Reute katika kanisa la mjini Aden lilioko juu ya jabali Hadid, alikwenda kukaa Tawahi akingoja safari yake ya Hambag, akaishi Ujerumani kufika mwaka 1870 mumewe akafa kwa ajali, kuainzia hapo bibi huyu akaanza kupata tabu ya kimaisha akawa hana msaada wa yeyote na watu wakamdharau katika kutapatapa kimaisha akanza kufuma na kutunga vitabu kikiwemo Memories of an-Arabian Prince,ingawa ulipofika mwaka 1922 alikumbukwa na alipelekewa mshahara wa paundi 100 kila mwaka  kutoka Unguja hayo ni mapesa mengi kwa wakati huo. Alizaa na mumewe watoto watatu wawili wanawake na mmoja wakiume.Salme aliwahi kuja Unguja kudai urithi wa baba yake kwa vile aliritadi ilikuwa hakuna sheria ya kuupata ,Ogasti 1885 alisusiwa na watu wote wa Zanzibar na watu walimfungia milango kila alipokwenda na kulisikika vilio, alipokelewa na muadhini wa mskiti wa mtoni na alimkumbatia akalia nae kwa kwikwi pia jamaa yake Mame Hamdani hakuweza kumdharau na wajarumani walikasirishwa kutokupewa urithi wake na walitaka kuipiga Zanzibar kwa Manuari tano za kijarumani Bismark,Stoch,Prince Adalber, Elizabeth na Gneisenan zikiongozwa na kepteni Commodore Paschen, zilizotia nanga bandarini na zingekuwa si hikma za Barghash ingekuwa hadith nyengine, zamani ikisemekana kupewa mimba kwa binti mfalme ni sababu za kisiasa zaidi wa jerumani walikuwa wakitaka ulwa kupitia kwake na Ujarumani ilipotaka kuzichukua nchi hizi za Afrika mashariki ilimtumia yeye kama chambo walitaka lazima apewe Bisalme paundi 20 elfu lakini akapewa Rupia elfu 80 tu na wakamlazimisha aondoe mkono wake katika miji ya usagara na witu wapate kuzitawala na Barghash akakubali kujiondoa ili Zanzibar ipate salama na huo ndio ukawa mlango wao wa kuingilia pande hizi za Afrika Mashariki na hata kakaitawala bara. Binti mfalme alikufa masikini  Febuari 1924 akiwa na umri wa miaka 82 nae ndo mtoto wa mwisho wa Sayed Said kufa baada ya kuhangaika nchi nyingi kama Lebanoni, Syria n.k. nahuo ndiyo ulikuwa mwisho wake kimaisha lakini hatoweza kusahaulika kimaandishi.

2 comments:

  1. Hii Historia ya Selme sio Kweli kwamba alikufa masikini.

    ReplyDelete
  2. Hii Historia ya Selme sio Kweli kwamba alikufa masikini.

    ReplyDelete